Baghdad: Mashambulio ya kujitoa mhanga yaendelea nchini Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad: Mashambulio ya kujitoa mhanga yaendelea nchini Iraq.

Nchini Iraq, watu watano wameuawa baada ya shambulio la bomu la kujitoa mhanga kwenye kituo cha polisi katika mji wa Hibhib, kaskazini mwa Baghdad.

Maafisa wa usalama wamesema watu kumi na watatu wamejruhiwa kwenye shambulio hilo.

Shambulio hilo lilikuwa limelengwa watu waliokwenda kupeleka maombi ya kazi ya polisi.

Shambulio hilo limetekelezwa siku moja baada ya mashambulio kadhaa yaliyotukia mjini Baghdad na kusababisha vifo vya watu zaidi ya sabini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com