1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulio mapya ya bomu yameutikisa mji mkuu wa Irak

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtT

Nchini Irak,washambulizi waliojitolea kufa wamejiripua kwenye kituo cha polisi cha kuandikisha watu kazi,kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.Hadi watu 28 wameuawa na zaidi ya 40 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.Mripuko mwingine wa bomu lililotegwa kando ya barabara uliwalenga polisi waliokuwa wakipiga doria mashariki mwa Baghdad.Shambulio hilo limeua Wairaki 4 na 1 alijeruhiwa.Mripuko wa pili asubuhi ya leo,ulitokea kwenye mkahawa mmoja mjini Baghdad.Ripoti zingine zinasema maiti 5 zenye ishara za kuteswa zimekutikana sehemu mbali mbali mashariki mwa mji mkuu Baghdad.Siku ya Jumamosi si chini ya Washia 10 walipigwa risasi na kuuawa baada ya mabasi madogo matatu kuvamiwa na watu wenye silaha,kusini mwa Baghdad. Inasemekana kuwa abiria wengine wapatao kama 50 walitekwa nyara.