BAGHDAD: Marekani yasema mabomu yaliojengwa Iran yatumiwa Irak
11 Februari 2007Matangazo
Wakuu wa majeshi ya Kimarekani nchini Irak, wanadai kuwa mabomu yaliojengwa Iran yanatumiwa na wanamgambo kushambulia vikosi vya Kimarekani. Kwa mujibu wa maafisa wa ulinzi,wa ngazi ya juu,tangu mwezi Juni mwaka 2004,si chini ya wanajeshi 170 wa Marekani na madola shirika wameuawa na zaidi ya 600 wamejeruhiwa kwa mabomu yaliotengenezwa Iran na kutumiwa Irak ambako hutegwa kando ya barabara.