1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Maliki atetea maendeleo ya serikali yake

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBR2

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki ametetea maendeleo yaliofikiwa na serikali yake katika kuleta utulivu nchini humo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa usalama mjini Baghdad Maliki hata hivyo amezishutumu nchi jirani na Iraq kwa kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi hiyo.Iraq na Marekani hususan wanazilaumu Iran na Syria kwa kutochukuwa hatua za kutosha kuzuwiya kuingizwa kwa silaha na wapiganaji nchini Iraq kwa kupitia mipaka yao.

Mkutano huo umefanyika siku moja kabla ya maafisa wawili wa kijeshi na wa kiraia wa Marekani kuwasilisha tathmini ya usalama kwa bunge la Marekani.

Generali David Petraeus anatazamiwa kutaja kupunguwa kwa umwagaji damu wa kimadhehebu kutokana na mkakati tata wa Marekani wa kuongeza wanajeshi wake nchini Iraq na kupendekeza kuongeza muda kwa wanajeshi hao kuendelea kuwepo nchini Iraq.