1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Makamu wa rais wa zamani wa Irak ahukumiwa kunyongwa

13 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSe

Makamu wa rais wa zamani wa Irak, Taha Yassin Ramadhan, amehukumiwa kunyongwa baaday a kupatikana na hatia kwa uhalifu dhidi ya binadamu. Makama kuu mjini Baghdad imempata Ramadhan na hatia kuhusiana na mauaji ya Washia 148 katika kijiji cha Dujail mnamo mwaka wa 1982.

Rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein na wapambe wake wawili wa ngazi ya juu katika serikali yake, walinyongwa kwa kuhusika katika mauaji hayo ya Dujail.

Wakati haya yakiarifiwa, watu takriban 75 wameuwawa na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa katika mashambuluio matatu ya mabomu mjini Baghdad.

Maofisa wa Irak wanasema mabomu yote matatu yalilenga masoko yanayomilkiwa na Washia na yaliripuriwa wakati mmoja wakati Washia walipokuwa wamenyamaa kimya kwa dakika chache kuadhimisha mwaka mmoja wa shambulio la bomu dhidi ya msikiti wa al Askari mjini Samarra.