1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Makampuni ya ulinzui yaondolewa kinga.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7B7

Baraza la mawaziri la Iraq limeidhinisha muswada wa sheria ambao unasitisha kinga ya kutoshitakiwa kwa makampuni ya kigeni yanayohusika na usalama yanayofanyakazi nchini humo.

Muswada huo utaondoa amri iliyotolewa na mamlaka ya utawala wa muda wa muungano wa nchi zinazoongozwa na Marekani nchini Iraq mwaka 2004 ambao ulitoa kwa wakandarasi wa kutoka mataifa ya nje kinga ya kutoshitakiwa nchini humo. Muswada huo wa sheria unabidi kupitishwa na bunge la Iraq. Hatua hiyo inakuja kutokana na tukio lililowahusisha walinzi wa usalama kutoka katika kampuni ya Kimarekani ya Blackwater mwezi uliopita ambapo watu 17 raia wa Iraq waliuwawa. Blackwater limesema kuwa walinzi wake walifanya hivyo katika misingi ya sheria. Kumekuwa pia na ripoti kuwa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imetoa kinga ya kiasi fulani ya kutoshitakiwa kwa wafanyakazi wa Blackwater.