1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kouchner ziarani Irak

20 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXS

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ufaransa, Bernard Kouchner, leo anatarajiwa kukutana na viongozi wa Irak wa jamii zilizogawanyika.

Bernard Kouchner, ni waziri mkuu wa kwanza wa Ufaransa kuitembelea Irak tangu uvamizi wa Irak ulioongozwa na Marekani ambao ulipingwa vikali na serikali ya Ufaransa.

Kiongozi huyo amepangwa kukutana na rais wa Irak, Jalal Talabani na mamakamu wake wawili, Tareq al Hashemi na Adel Abdel Mahdi. Waziri Kouchner pia atakutana na rais wa eneo la kaskazini la Wakurdi, Massud Barzani.

Alipowasili mjini Baghdad hapo jana waziri Kouchner aliahidi kwamba Ufaransa itaisidia Irak kumaliza machafuko yanayoendelea nchini humo, hatua inayoashiria juhudi mpya za kuboresha uhusiano kati ya Ufaransa na Marekani.