1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Kikosi cha Marekani tayari kuwekwa Iraq

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYw
Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change MDC Morgan Tsvangirai
Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change MDC Morgan TsvangiraiPicha: AP

Uwekaji wa kwanza wa kikosi cha ziada cha Marekani mjini Baghdad kama ilivyoahidiwa na Rais George W Bush kiko njiani kupelekewa nchini Iraq.

Zaidi ya wanajeshi 3,000 wanatazamiwa kuanza opereshenui zao ifikapo tarehe Mosi mwezi wa Februari.Hicho kitakuwa ni kikosi cha utangulizi cha wanajeshi wa ziada 21,000 watakaopelekwa nchini Iraq na Bush ikiwa ni sehemu ya mkakati wake mpya aliouzinduwa mapema mwezi huu.

Uwekaji wa wanajeshi hao unaandamana na umwagaji damu zaidi wakati jeshi la Marekani likitangaza vifo vya wanajeshi watano katika jimbo la Anbar na kufanya idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa hapo Jumamosi kufikia 22.

Katika mji wa kusini wa Basra mwanajeshi mmoja wa Uingereza ameuwawa na wengine wanne kujeruhiwa na bomu lililotegwa barabarani.