1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Jeshi la Marekani ladai wanajeshi zaidi Iraq

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChP

Wanajeshi wa Marekani walioko nchini Iraq wamemwambia waziri mpya wa ulinzi wa Marekani Robert Gates kwamba vikosi zaidi vya Marekani vinahitajika kukomesha umwagaji damu nchini humo na kuwapa muda vikosi vya usalama vya Iraq kujiimarisha zaidi.

Kufuatia kuapishwa kwake siku nne zilizopita Gates yuko ziarani nchini Iraq kushauriana na makamanda wa kijeshi na viongozi wa Iraq wakati Rais George W. Bush wa Marekani akisubiri mapendekezo yake kabla ya kutangaza mkakati mpya kwa Iraq hapo mwezi wa Januari.

Umwagaji damu unaendelea nchini humo ambapo hapo jana shambulio la kujitolea muhanga maisha limeuwa Wairaq 13 waliokuwa wakiwasili katika kituo cha kujiandika polisi katikati ya Baghdad na wanawake wawili wameuwawa katika shambulio jengine tafauti la mzinga kwenye soko kusini magharibi mwa Baghdad.