1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Jeshi la Iraq linaweza kulinda usalama

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBim

Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki amesema leo kwamba jeshi la Iraq na polisi yana uwezo wa kulinda usalama nchini humo wakati vikosi vya Marekani vitakapoondoka wakati wowote ule juu ya kwamba amekiri kwamba wanajeshi wake wanahitaji silaha zaidi na mafunzo.

Al Maliki amesema serikali yake inahitaji muda kutekeleza malengo ya kisiasa inayotaka serikali ya Marekani na amesisitiza kwamba ni jambo la kawaida kabisa kwamba kufikia maendeleo nchini humo ni jambo gumu kwa kuzingatia umwagajji damu ulioko na kutofautina miongoni mwa viongozi wake.

Amewaambia waandishi wa habari bila ya kutaja tarehe ya kuondowa vikosi vya Marekani kutoka Iraq kwamba wanahitaji muda na juhudi hususan kwa kuwa mchakato huo wa kisiasa unakabiliwa na shinikizo la masuala ya usalama,uchumi na huduma kadhalika uingiliaji kati wa nchi za eneo hilo na wa kimataifa.