1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Bomu laua watu 26 katika mtaa wa maduka ya vitabu.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM9

Bomu limelipuka katika mtaa wenye maduka mengi ya vitabu mjini Baghdad na kuuwa watu 26 na kusababisha kuungua moto kwa maduka kadha na magari hii leo.

Polisi wamesema kuwa mlipuko huo katika mtaa wa Mutanabi umeua watu 26 na kuwajeruhi wengine 54.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa mlipuko huo umesababishwa na mtu aliyejitoa muhanga.