1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Blair afanya ziara ya ghafla Iraq

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0S

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair alioko njiani kun’gatuka amefanya ziara ya ghafla mjini Baghdad ikiwa ni msaaa machache tu baada ya kushutumiwa vikali na Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter.

Baada ya mazungumzo na maafisa waandamizi wa serikali ya Iraq katika eneo la Kanda ya Kijani lenye ulinzi mkali yalioko makao makuu ya serikali Blair amesisitiza kwamba hali nchini Iraq imeanza kuwa nzuri miaka minne baada ya kun’golewa kwa dikteta Saddam Hussein.

Lakini Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter ameiambia radio ya taifa ya Uingereza kwamba hatua ya Blair kuunga mkono mbinu za Bush kwa Iraq imekuwa ya kutofikiria na ya unyenyekevu na kusababisha kile Carter alichokiita maafa makubwa ambayo yamevirefusha vita vya Iraq.Carter pia ameushambulia urais wa George W. Bush kuwa mbaya kabisa katika historia ya ushirikiano wa kimataifa.

Katika jimbo la Diyala nchini Iraq wapiganaji waliovalia sare za kijeshi wamewachaguwa wanaume 15 wa Kikurdish na kuwauwa katika kijiji kimoja.

Wakati huo huo jeshi la Marekani linasema wanajeshi wanane wameuwawa tokea Ijumaa nchini kote Iraq.