1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Askari wa Marekani auawa nchini Iraq

Askari mmoja wa Marekani ameuawa mjini Baghdad wakati watu wenye silaha walipokishambulia kikosi cha jeshi la Marekani kilichokuwa katika doria.

Jeshi la Marekani limesema kuwa watu hao wenye silaha waliwashambulia ghafla askari hao wa Marekani huko magharibi mwa Bahdad na kumuua askari huyo..

Kuawa huko kunaongeza idadi ya askari wa Marekani waliyoauawa nchini Iraq toka ilipoivamia nchi hiyo miaka minne iliyopita kufikia zaidi ya elfu tatu na mia mbili.

Wakati huo huo askari wa Marekani aliyopatikana na hatia ya kumbaka binti wa Kiiraq wa miaka 14 kabla ya kuiua familia ya binti huyo, amehukumiwa kifungo cha miaka 2.

Askari huyo Bryan Howard mwenye umri wa miaka 20 alihukumiwa na mahakama ya Kentucky kwa kosa hilo alilotenda mwaka jana huko kusini mwa Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com