BAGHDAD: Askari polisi waliotekwa nyara wameuawa | Habari za Ulimwengu | DW | 03.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Askari polisi waliotekwa nyara wameuawa

Maiti za askari polisi 14 wa Kiiraki zimekutikana kaskazini-mashariki ya mji mkuu Baghdad,siku moja baada ya kuripotiwa kuwa walitekwa nyara na wanamgambo.Msemaji wa wizara ya ndani ya Irak, amethibitisha kuwa maiti hizo ziligunduliwa katika wilaya ya Diyala.Kundi la waasi wenye mahusiano na Al-Qaeda limesema,liliwateka nyara na kuwaua askari polisi hao,kulipiza kisasi kitendo cha kumbaka mwanamke mmoja wa madhehbu ya Kisunni.Kwa upande mwingine,bomu la gari lililoripuka katika soko lililojaa watu huko Sadr City,ukingoni mwa mji mkuu Baghdad,limeua si chini ya watu 10 na wengine 17 wamejeruhiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com