1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Amri ya kuzuia kutoka majumbani yaondoshwa

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqu

Serikali ya Iraq imeondosha amri ya kuzuia watu kutoka majumbani mwao katika mji mkuu Baghdad na mji wa kusini,Basra.Amri ya kuzuia watu kutembea mitaani ilitangazwa baada ya shambulio la bomu kuteketeza kuba la dhahabu na minara miwili ya msikiti mashuhuri wa madhehebu ya Kishia mjini Samarra.Baada ya shambulio hilo,msikiti wa madhehbu ya Kisunni pia ulishambuliwa mjini Basra.Ripoti zinasema,serikali ya Iraq na Shirika la UNESCO la Umoja wa Mataifa,zimeamua kuutengeneza msikiti wa dhahabu ulioteketezwa mjini Samarra.