BAGHDAD : Al-Maliki ataka Blackwaters itoke Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Al-Maliki ataka Blackwaters itoke Iraq

Waziri wa Iraq Nuri al Maliki ameitaka wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuitowa kampuni ya Blackwater kutoka nchini Iraq kwa sababu kampuni hiyo ya ulinzi ya kibinfasi ya Marekani kufyetua risasi kusikokuwa na haja na kuwauwa raia wa Iraq.

Mshauri wake Sami al Askari amesema serikali ya Iraq imekamilisha uchunguzi wake kwa mauaji ya Septemba 16 na imeridhika kabisa na matokeo kwamba kufyetuliwa kwa risasi na kampuni hiyo kumefanyika bila ya uchokozi.

Walinzi wa kampuni ya Balckwaters waliokuwa wakilinda msafara wa kidiplomasia wa Marekani walifyetuwa risasi hizo wakati wakisafiri kwenye kitongoji cha hatari mjini Baghdad na kuuwa raia 17.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com