1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan yafanya luteka za kijeshi na Uturuki

Lilian Mtono
23 Oktoba 2023

Wizara ya ulinzi ya Azerbaijan imesema wameanza luteka ya pamoja ya kijeshi pamoja na mshirika wake Uturuki karibu na mpaka wa Armenia.

https://p.dw.com/p/4Xv2b
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev akibusu bendera ya nchi yake
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev akibusu bendera ya nchi yakePicha: Azerbaijani Presidency/Anadolu/picture alliance

Luteka hizo zinafanyika ikiwa ni wiki chache baada ya Baku kurejesha udhibiti wa mkoa wa Nagorno-Karabakh kutoka kwa Waarmenia waliojitenga.

Wizara hiyo imesema hadi wanajeshi 3,000 watashiriki luteka hizo zinafanyika katika eneo la Nakhichevan lililoko kati ya Iran na Armenia pamoja na maeneo yaliyorejeshwa kutoka kwa Waarmenia waliojitenga.

Soma pia;Azerbaijan yapeperusha bendera ya taifa lake Karabakh

Luteka hizo zinafanyika wakati Azerbaijan, Armenia, Uturuki, Iran na Urusi wakiwa wamejiandaa kuwatuma mawaziri wao wa nje kwa mazungumzo mjini Tehran katika mfumo wa kidiplomasia, yaliyoanzishwa na Moscow mwaka 2020, baada ya Baku na Yerevan kupigana wakizozania eneo la Nagorno-Karabakh.

Mazungumzo hayo yanachukuliwa kama jaribio la Urusi kupunguza ongezeko la ushawishi wa magharibi kwenye eneo inalilolichukua kama himaya yake.