1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS: Washukiwa waliosababisha moto wafunguliwa mashtaka

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVC

Polisi nchini Ugiriki wamewafungulia mashtaka washukiwa saba waliowacha mioto iliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 63 nchini humo.

Eneo lililoathirika zaidi kutokana na moto ni la Pelpponnese kusini mwa mji mkuu Athens, ambako maafisa waliwahamisha maelfu ya watu kutoka madarzeni ya vijiji.

Vikosi vya kimataifa vya wazima moto na vifaa vimepelekwa katika eneo hilo kukabiliana na mioto hiyo.

Wakati huo huo, serikali ya Ugiriki imetenga euro milioni 200 kuzisaidia na misaada ya dharura jamii zilizoathirika.