1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS: Wafaransa waendelea kutafutwa

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBr

Wanajeshi wa jeshi la maji nchini Ugiriki wanaendelea kuwatafuta abiria wawili Wafaransa waliopotea wakati wa kuwahamisha abiria waliokuwa ndani ya meli iliyozama karibu na kisiwa cha Ugiriki.

Jeshi linaloilinda pwani ya Ugiriki limesema linachukua pia hatua za dharura kuzuia mafuta kumwagika kutoka kwa meli hiyo na kuingia baharini.

Meli hiyo ijulikanayo kwa jina ´Sea Diamond´ iligonga mwamba karibu na kisiwa cha Santorini Alhamisi iliyopita na kusababisha operesheni kubwa ya kuwaokoa abiria 1,600 pamoja na wafanyakazi waliokuwa ndani ya meli hiyo.