ATHENS : Moto yaendelea kuwaka kwenye misitu Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 29.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ATHENS : Moto yaendelea kuwaka kwenye misitu Ulaya

Moto kwenye misitu inaendelea kuwaka katika sehemu kadhaa za kusini na kusini mashariki kwa Ulaya ambazo zimekuwa zikikabiliwa na wimbi la joto kubwa katika kipindi cha wiki chache zilizopita.

Ugiriki ndio iliothairika zaidi ambapo vikosi vya zima moto vimekuwa mbioni kudhibiti moto mkubwa wa misitu. Hali ya hatari imeendelea kubakia katika sehemu kadhaa za kusini mwa Italia.

Wakati huo huo Uingereza na Wales zinaendelea kukabiliwa na mvua kubwa zaidi ambazo zimetabiriwa kunyesha mwishoni mwa juma hali hiyo inakuja baada ya maji kuanza kupunguwa katika sehemu fulani za Uingereza ambazo zimekumbwa na mafuriko mbaya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miongo kadhaa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com