ATHENS: Maelfu ya watu waandamana kupinga vyuo vikuu vya kibinafsi nchini Ugiriki. | Habari za Ulimwengu | DW | 18.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ATHENS: Maelfu ya watu waandamana kupinga vyuo vikuu vya kibinafsi nchini Ugiriki.

Maandamano yameendelea mjini Athens, Ugiriki ambapo waandamanaji wameteketeza magari na kukabiliana na polisi wa kuzima ghasia.

Maandamano hayo yameandaliwa na wanafunzi wanaopinga vyuo vya kibinafsi kuruhusiwa kuanza kufundisha nchini humo.

Ghasia hizo zilizuka tangu jana wakati maelfu ya waandamanaji walipokuwa wakielekea bungeni ambako wabunge walikuwa wakijadili suala hilo.

Nje ya jengo la bunge, vijana waliwavurumishia mawe polisi huku polisi naowakiwarushia gesi ya kutoa machozi.

Waandamanaji hao wanadai hatua hiyo itasababisha gharama ya masomo kupanda hadi ya watu maskini kushindwa kuyagharamia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com