ASTANA : Steinmeir ziarani Asia ya Kati | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ASTANA : Steinmeir ziarani Asia ya Kati

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir ametowa wito wa kufanyika kwa mageuzi kabambe ya kisiasa katika Asia ya Kati.

Kufuatia kuwasili kwake katika mji mkuu wa Kazakhstan wa Astana Steinmeir amesema kuongeza uwekezaji wa Ujerumani katika eneo hilo kutafungamanishwa na maendeleo yanayofikiwa katika utawala wa sheria.Kazakhstan ni kituo cha kwanza cha ziara hiyo ya Steinmeir katika Asia ya kati ambayo pia itamfikisha Uzbekistan,Turkmenistan,Tadjikistan na Kyrgzstan.

Ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Ujerumani kushika wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya hapo mwezi wa Januari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com