ASMARA:Mkutano wa kupinga uvamizi wa Etrhiopia waendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 06.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ASMARA:Mkutano wa kupinga uvamizi wa Etrhiopia waendelea

Takriban washiriki 300 wakiwemo viongozi wa vyama vya kiislamu na wanachama wa upinzani nchini Somalia wanaopinga kuwepo majeshi ya Ethiopia nchini mwao wanahudhuria mkutano unaolenga kuanzisha muungano utakaopambana na uvamizi wa Ethiopia nchini Somalia unaofanyika mjini Asmara nchini Eritrea.

Mkutano unafanyika kama ishara ya kupinga mkutano wa maridhiano uliomalizika mjini Mogadishu bila ya kufahamisha yaliyoafikiwa.

Mkuatano wa mjini Mogadishu ulihudhuriwa na washiriki 2000 kutoka koo mbali mbali, wawakilishi wa serikali ya mpito, mashirika yasiyo ya kiserikali.

Umoja wa mataifa, Ujumbe wa nchi za kiarabu, Umoja wa Ulaya na wawakilishi wa umoja wa Afrika wanahunduria mazungumzo hayo ya mjini Asmara.

Suleiman Roble mtayarishi wa mkutano huo amesema kwamba wawakilishi wa makundi ya kikabila wameususia mkutano huo kwa madai kwamba hauwawakilishi Wasomali wote.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com