Askari wa NATO wafa Afghanistan
7 Januari 2008Matangazo
KABUL:
Wanajeshi wawili wa kikosi cha NATO kilichoko Afghanistan,wauawa baada ya gari lao kupinduka.
Kisa hicho kimetokea katika kijiji kimoja kilichoko eneo la machafuko la kusini.Taarifa ya ushirika imesema kuwa jali hiyo imetokea jana jumapili katika wilaya ya Zhari katika mkoa wa Kandahar ambako ndio kitovu cha wapiganaji wa Taliban.Taarifa haikutoa uraia wa wanajeshi hao lakini jeshi la kulinda amani la Nato sehemu za Kandahar huwa linalota Canada.