1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Askari sita wa Mali wauawa katika shambulizi la "kigaidi"

Bruce Amani
13 Agosti 2023

Jeshi la Mali limesema wanajeshi wake sita wameuwawa katika shambulizi la Ijumaa lililofanywa na "makundi ya kigaidi" katika mji wa Ber Kaskazini mwa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4V7Jy
Mali Unruhen Soldaten
Picha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Jeshi la Mali limesema wanajeshi wake sita wameuwawa katika shambulizi la Ijumaa lililofanywa na "makundi ya kigaidi" katika mji wa Ber Kaskazini mwa nchi hiyo. Idadi hiyo ya vifo imetangazwa kuongezeka leo baada ya taarifa ya awali ya Ijumaa kusema kuwa mwanajeshi mmoja aliuwawa na wengine wanne walijeruhiwa.

Soma pia: Marekani yaweka vikwazo kwa baadhi ya maafisa wa Mali

Taarifa ya jeshi hilo imeongeza kuwa makundi hayo ya kigaidi yaliitelekeza miili 24 ya wanamgambo, bunduki kadhaa aina ya AK-47 pamoja na pikipiki. Mapambano yaliyosababisha mauaji hayo yalitokea  baada ya " jaribio la uvamizi na ufyatuaji wa risasi" uliofanywa na makundi ya kigaidi dhidi ya jeshi la Mali.

Wanajeshi wa Mali wako kwenye mchakato wa kupelekwa Ber kama sehemu ya makabidhiano wakati wanajeshi wa kulinda amani nchini humo MINUSMA wakijiandaa kuondoka kwenye taifa hilo. Uongozi wa kijeshi ulioingia madarakani mwaka 2020, ulilishinikiza Baraza la Usalama la Umoja Wa Mataifa liondoe ujumbe huo wa kulinda amani kufikia mwishoni mwa mwaka huu.