1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASHGABAT: Wapiga kura wachagua rais mpya nchini Turkmenistan

11 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTB

Wapiga kura nchini Turkmenistan katika Asia ya Kati hii leo wamepiga kura kumchagua rais mpya.Wagombea sita wanawania nyadhifa ya urais,kufuatia kifo cha marehemu Sapamurat Niyasov.Inaaminiwa kuwa rais wa mpito Gurbanguly Berdymushammedov anaeungwa mkono na serikali, atashinda uchaguzi wa leo.Turkmenistan,ambayo hapo awali ilikuwa jumuiya mojawapo katika Soviet Union ya zamani ina akiba kubwa ya gesi.Si hilo tu bali hata kimkakati,nchi hiyo inayopakana na Afghanistan na Iran ina umuhimu mkubwa.Niyasov aliefariki Desemba mwaka jana aliiongoza nchi hiyo kwa mabavu.