Arsenal yaisambaratisha Chelsea
28 Desemba 2010Matangazo
Yalikuwa ni mabao ya Alex Song, Cesc Fabregas na Theo Walcott yaliyopeleka majonzi Stamford Bridge.
Arsenal sasa imefikisha pointi 35, nyuma ya vinara Manchester United wenye pointi 37, huku Chelsea ikibakia katika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 31.
Kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti alikiri kuwa hali si nzuri kwao, na kwamba ni lazima waamke, ingawaje hana wasiwasi.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters
Mhariri:Josephat Charo