1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

APR FC ya Rwanda yanyeshewa mvua ya magoli

2 Oktoba 2023

Timu ya jeshi la Rwanda APR FC imetupwa nje baada ya kunyeshewa mvua ya magoli na Club ya Pyramid ya Misri magoli 6-1 jijini Cairo katika kinyang'anyiro cha kusaka tikiti ya kufuza makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

https://p.dw.com/p/4X3fN
Fussball Champions League | RB - Young Boys
Mpira ukitikisa wavuPicha: Denis Balibouse/REUTERS

 

Awali mchezo wa mzunguko  wa kwanza timu zote zitoka sare ya bila kwa bila. Huu ukiwa ni mfululizo wa miaka nenda rudi ikishindwa kutinga makundi.

Soma pia: Rayon Sport yashindwa kutamba katika ligi kuu Rwanda

Kwa upande mwingine Rayon  sport mwakilishi wa Rwanda katika  mashindano ya Shirikisho pia imeshindwa kusonga hatua ya makundi ya CAF Confederation baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-2 na AL Hilal katika uwanja wa Pele.

Kocha wa timu ya Rayon sport alikuwa na haya ya kusema baada ya mechi  hiyo

‘'Nasikitika sana  kwasababu nilikuja hapa kwa ajili ya kufuzu  kwenye makundi ili kurejesha ndoto za mashabiki, wapenzi na timu. Nashukuru sana kwa  mashabiki amabao  wamejitokeza kwa wingi, Rayon ni timu ni nzuri, tumecheza vizuri lakini katika soka bahati pia ni muhimu sana,  leo hatukuwa na bahati  sasa hatukufuzu ndivo ilivo Bwana''

Mechi ya mzunguko wa kwanza mjini Cairo  Arab contractors ilifunga mabao 2-1 mchezo wa marudio Kigali timu hizo zikatoka sare tasa. Rayon ikaaga mashindano ya kombe la Afrika

Mwalimu Muhamed Ouda kutoka Misri  anayekinoa kikosi cha AL Hilali ya Libya akijigamba baada ya kuwanyuka Rayon kwa njia ya matuta, amesema si mara ya kwanza kuibandua Rayon mashindanoni.

‘' Mwaka 1996 nilikuwa nikiichezea  timu ya Arab contractors  tuliwafunga Rayon mabao 2-1 mjini Cairo  halafu mchezo wa marudiano katika uwa wa Kigali  tukatoka tasa''.