Annapolis | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Annapolis

Annapolis ni vishindo vya darini vilivyoishia sakafuni

default

Ehud Olmert

Mkutano wa amani ya mashariki ya kati wa Annapolis ni “vishindo vya darini vilivyoishia sakafuni.”:Matokeo yake juu ya maswali hasa yanayowatenganisha wapalestina na waisraeli kama vile kuundwa dola la wapalestina na amani ya kudumu, yaliondokea ahadi tupu .

Mkutano ulitaja wakati tu wa kuhetimisha mazungumzo lakini sio kuyatatua matatizo..Kwahivyo, mkutano wa Annapolis, umeleta mabadiliko machache tu kutoka hali ilivyokua hadi sasa.

Mkutano wa kilele uliohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi na mashirika hadi 50 huko Annapolis,Maryland chini ya rais George Bush uliitishwa kujadili utaratibu wa hatua kwa hatua kujenga amani katika Mashariki ya Kati baina ya Israel na jirani zake wa kiarabu kwa kuunda dola jipya Mashariki ya kati.

Akizungukwa na waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel na rais wa mamlaka ya ndani ya wapalestina Mahmud Abbas,Bush alisoma taarifa ya pamoja ilioafikiwa na viongozi hao 2.Wachunguzi wengi hawakuami ni kwamba taarifa kama hiyo ingetolewa kutokana na tofauti zilizobakia juu ya hatima ya miwsho ya wapalestina kuhusu kuundwa kwa dola lao.

Taarifa hii ilibainisha moja ya dalili chache madhubuti kuwa sasa maendeleo yanafanyika –tangazo la kuundwa kwa kamati itakayoongoza shughuli za kuundwa kwa dola la wapalestina na mikutano ya kila baada ya wiki 2 baina ya waziri mkuu Olmert na Bw.Mahmud Abbas.Rais Bush akanadi kwamba kamati hiyo itakua na kikao chake cha kwanza hapo Desemba 12.

Juu ya hivyo, tofauti nyingi za kimsingi baina ya mahasimu hawa 2 zimesalia pale pale na baadhi ya wakati zimedhihirika wakati wa hotuba za Bw.Olmert na Bw.Abbas.

Bw.Olmert alianza hotuba yake kwa kuhesabu tena idadi ya mabasi,mikahawa na vituo vya mapumziko vilivyoripuliwa na aliewaita magaidi wa kipalestina wakati yeye alipokuwa diwani mkuu wa Jeruselem.Olmert pia alioungama kuwa hali ya wakimbizi ya wapalestina inachangia katika uadui dhidi ya Israel huko Palestina.Akasema sio Israel haijali hisia hizo.

Kwa upande wake, rais Bush akitumai kwa mkutano huu wa Annapolis, angeweza kupambana na siasa kali iliotanda mashariki ya kati.Akitumai pia kwa kushiriki kwa nchi nyingi za kiarabu,hii ingechangia kutoa sura bora ya Marekani katika Mashariki ya Kati na hasa katika kupunguza ushawishi unaokua wa Iran.

Hata msimamo huu wa Marekani umekosolewa.wakoasoaji wanadai Marekani huchukua tu juhudi katika utaratibu wa amani wa Mashariki ya kati ikiwa unainufaisha binafsi.Mfano 2003 Marekani ilikataa kuidhinisha ramani ya Roadmap kuelekea amani wakati ikishughulika zaidi kutaka kuungwamkono uvamizi wake nchini Iraq.

Chama cha HAMAS kinachoungwa mkono na Iran, hakikualikwa kabisa katika mkutano wa Annapolis ingawa kina sehemu ya madaraka na chama cha Fatah cha Mahmud Abbas.Hamas kilifanya maandamano makubwa huko Gaza na kuhujumu suluhu yoyote itakayofungwa na Israel.Kiongozi wa Hamas,Ismail Haniya,amesema ardhi yote kutoka bahari ya Mediterranian hadi mto Jordan irejeshwe mikononi mwa wapalestina.Akaongeza “na hatutaitambua Israel.”

Syria iliojiunga mwishoni na mkutano wa Annapolis na licha ya kuiungamkono Hamas-na kutokua na uhusiano wa kibalozi na Israel-inaonersha kuzidi kutengwa kwa hamas.Syria binafsi ilikosolewa na Iran kwa kushirikiana na Israel.

Kwahivyo, ikionekana kwa sasa mnyemeleano wowote baina ya Israel na Marekani upande mmoja na Syria na nchi nyengine za kiarabu upande wapili, ni vigumu na juhudi ya rais Bush kujenga ushirika dhidi ya Iran kupitia utaratibu wa amani wa Mashariki ya kati, itakabiliwa na pingamizi sawa na ile iliopata katika Roadmap.

Saudi Arabia ambayo pia ilishiriki Annapolis, waziri wake wa nje Saud Al Faisal, alibainisha wazi kwamba Saudia, haina nia wakati huu ya kusawazisha uhusiano na Israel na kwamba hangepeana mkono na waziri mkuu Olmert.

 • Tarehe 28.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUEe
 • Tarehe 28.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUEe

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com