ANKARA:Uturuki na Irak kushirikiana kuliangamiza kundi la Kikurdi la PKK | Habari za Ulimwengu | DW | 08.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA:Uturuki na Irak kushirikiana kuliangamiza kundi la Kikurdi la PKK

Uturuki na Irak zimekubaliana kushirikiana dhidi ya kundi la Wakurdi waliojitenga la PKK linalo kalia maeneo ya kaskazini mwa Irak.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza makubaliano hayo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kati yake na waziri mkuu wa Irak Nuri al Maliki mjini Ankara.

Uturuki imekuwa ikiishinikiza Irak kuwasaka wafuasi wa Kikurdi kundi la PKK ambao wanadaiwa kuwa ni magaidi la sivyo Uturuki imekuwa ikitishia kutmia nguvu za kijeshi kuwasaka wafuasi wa kundi hilo.

Mjumbe wa Kikurdi Mahmoud Othman amesema ana imani kubwa kwamba waziri mkuu wa Irak Nuri al Maliki ataishawishi Uturuki kumaliza mzozo wa kundi la PKK kwa njia ya mazungumzo.

Uturuki imekuwa ikipambana na kundi la PKK na Wakurdi kwa muda wa miaka 25 nchi hiyo imeweka majeshi yake katika mpaka wake na Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com