1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Waziri mkuu kuondoa marufuku ya uvaaji wa hijab.

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOQ

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameliambia gazeti la Finacial Times kuwa anataka kuondoa marufuku dhidi ya uvaaji wa hijab katika vyuo vikuu nchini humo.

Matamshi yake hayo yananzisha upya hali ya mvutano na wale wanaopendelea mtengano baina ya serikali na dini, ikiwa ni pamoja na majenerali wa jeshi la nchi hiyo, ambao wanashaka kuwa Erdogan anataka kuimarisha jukumu la dini nchini Uturuki. Marufuku ya kuvaa hijab nchini Uturuki katika ofisi za serikali na vyuo vikuu, hatua ambayo inatekelezwa na jeshi, ni moja kati ya matokeo ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1980.