1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA : Uturuki yakataa mapendekezo ya Iraq

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CP

Uturuki hapo jana imeyakataa mapendekezo ya Iraq kuwazuwiya waasi wa Kikurdi kuvuka mpaka na kuishambulia Uturuki kuwa hayatoshelezi na yamechelewa mno na kwamba nchi hiyo inaendelea kuwa kwenye hali ya hatari.

Kufuatia mkutano na ujumbe wa Iraq katika mji mkuu wa Uturuki Ankara wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imetowa taarifa yenye kusema kwamba mapendekezo hayo yatachukuwa muda mrefu kutekelezwa.Imesema Uturuki inaitaka serikali ya Iraq kuchukuwa hatua za dharura na madhubuti kuwazuwiya waasi wa PKK kuwashambulia wanajeshi wa Uturuki kwa kupitia ardhi ya Iraq.

Wakati huo huo maelfu kwa maelfu ya wanajeshi wa Uturuki inasemekana kuwa wamewekwa kwenye mpaka wa nchi hiyo na Iraq katika maandalizi ya uwezekano wa kuingia kaskazini mwa Iraq kuwatokomeza waasi hao wa Kikurdi.