Ankara: papa Benediokti XV1 awasili Uturuki | Habari za Ulimwengu | DW | 28.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara: papa Benediokti XV1 awasili Uturuki

Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani Benedikti XV1 amewasili nchini Uturuki kwa ziara nyeti ya siku nne. Alipoondoka Roma kuelekea Ankara, kiongozi huyo wa kidini alisema ziara yake ina lengo la kuboresha maelewano baina ya Wakristo na Waislamu. Papa Benedikti aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Ankara, kukiwa na ulinzi mkali, kwa mazungumzo ya kwanza na Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Mjini Istanbul maelfu ya Waturuki waliandamana siku ya Jumapili kupinga ziara hiyo. Kiongozi huyo mkuu wa kanisa Katoliki duniani alizusha hasira miongoni mwa Waislamu mwezi Septemba, alipoihusisha dini ya Kiislamu na matumizi ya nguvu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com