ANKARA: Mageuzi ya Katiba yaidhinishwa na Bunge la Uturuki | Habari za Ulimwengu | DW | 01.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA: Mageuzi ya Katiba yaidhinishwa na Bunge la Uturuki

Bunge la Uturuki kwa mara ya pili limeidhinisha kufanya mageuzi katika Katiba ya nchi.Kuambatana na mageuzi hayo,rais wa nchi atachaguliwa moja kwa moja na raia badala ya kuchaguliwa na bunge. Rais Ahmet Necdet Sezer alipinga mageuzi hayo, yalipopitishwa na bunge kwa mara ya kwanza,lakini hatoweza kufanya hivyo mara ya pili.Kwa upande mwingine anaweza kuitisha kura ya maoni kuamua mageuzi hayo ya Katiba.Chama tawala cha Uturuki chenye itikadi za Kiislamu,kilipendekeza kufanya mageuzi hayo kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo,tangu bunge kukataa kumuidhinisha mjumbe aliechaguliwa na serikali kugombea urais katika uchaguzi ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com