AMSTERDAM: Polisi wawakamata watu 6 watuhumiwa wa mtandao mpya wa kigaidi wa kiislamu
7 Novemba 2006Matangazo
Polisi nchini Uholanzi wamewakamata watu 6 wanaotuhumiwa kuwajiri watu wa kujitolea katika vita vya jihad. Watuhumiwa hao sita, wanamume watano na mwanamke moja, sasa wametiwa ndani mjini Amsterdam mapema leo asubuhi. Wendeshamashitaka nchini Uholanzi wamesema kukamatwa watu hao ni matokeo ya uchunguzi juu ya mtandao wa kimataifa wa magaidi wa kiislamu ulioanzishwa mwezi Novemba mwaka 2005. Watatu miongoni mwa watuhumiwa hao, walikwenda nchini Azerbaijan katika mafunzo ya vita vya jihad. Walikamatwa huko na kurudishwa nchini Uholanzi. Watuhumiwa hao 6 wanatarajiwa kuhojiwa na jaji baadae wiki hii ambapo itaamuliwa iwapo wasalie ndani.