1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN. Rice yuko Jordan katika ziara ya mashariki ya kati

26 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFA

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice yuko mjini Amman, Jordan katika ziara inayoylenga kufufua mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati.

Mara tu aliposwasili bibi Rice alifanya mazungumzo na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas kabla ya mkutano wake na mfalme Abdullah wa pili wa Jordan.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ambae pia anazuru mashariki ya kati amesema Akiwa mjini Ramalla kuwa hatakutana na viongozi wa serikali ya chama kinachotawala cha Hamas katika maeneo ya Palestina.

O ton……Kwa wakati huu sitokuwa na fursa ya kukutana na waziri mkuu Ismail Haniya au mawaziri wengine wa Palestina …..nafikiri kuwa hali ya kisiasa bado haijatengemaa vyema.

Lakini ujumbe wangu kwa Israel ni kwamba nina hakika kuwa rais Mahmud Abbas yuko tayari kushirikiana katika kutafuta suluhisho la amani.

Akiwa mjini Ramallah katibu mkuu amesema kuwa upo uwezekano wa Israel kushiriki katika mkutano wa nchi za kiarabu ijapokuwa hakuna hakikisho iwapo mualiko utatolewa kwa Israel. Ijapokuwa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kuwa hatasita kuhudhuria mkutano huo ikiwa ataalikwa.