AMMAN : Mfalme Abudullah ataka Marekani ichukuwe hatua | Habari za Ulimwengu | DW | 03.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AMMAN : Mfalme Abudullah ataka Marekani ichukuwe hatua

Mfalme Abdullah wa Jordan hapo jana ameitaka Marekani kuchukuwa hatua hivi sasa kuboresha taswira yake huko Mashariki ya Kati na kuitaka Israel kuachana na fikra ya kujijengea ngome ya kujilinda.

Abdullah ambaye alikuwa akizungumza kabla ya ziara yake inayokuja nchini Marekani pia ameonya kwamba Mashariki ya Kati imesimama katika hatua muhimu sana.Ameiambia televisheni ya taifa nchini Jordan kwamba wanakabiliana na mambo mawili ya kuchaguwa amani na utulivu au machafuko.

Abdullah anatarajiwa kukutana na Rais George W. Bush wa Marekani na kulihutubia bunge la Marekani wiki ijayo ambapo atatea uhusiano wake na Marekani huku kukiwa na shutuma dhidi ya ziara yake hiyo huko nyumbani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com