Amirijeshi abadilishwa Iran
2 Septemba 2007Matangazo
TEHERAN:
Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran,Ayatollah Ali Khamenei, amembadilisha kamanda wa Jeshi la kimapinduzi humo nchini.Kituo cha TV cha Iran kimeripoti kwamba amirijeshi-mkuu wa zamani Yahya Rahim Safavi nafasi yake inachukuliwa sasa na Mohammad Ali Jaafari.
Hakuna sababu kwanini mabadiliko hayo yanafanyika.
Jeshi la walinzi wa mapinduzi liliundwa muda mfupi baada ya mapinduzi ya kiislamu ya 1979.