Aliyekuwa nahodha wa Man United Vidic astaafu
29 Januari 2016Matangazo
Vidic alishinda mataji matano ya Premier League na Kombe la Mabingwa Ulaya mwaka wa 2007-2008 wakati wa miaka yake minane uwanjani Old Trafford, lakini akakumbwa na majeraha yaliyomlazimu kuamua kuzitundika njumu.
Mserbia huyo aliruhusiwa kuondoka klabu yake ya Inter Milan mapema mwezi huu baada ya kipindi cha miezi 18 nchini Italia iliyojaa majeraha. Vidic alijiunga na United akitokea Spartak Moscow mnamo Januari 2006 na akaweka ushirikiano imara katika safu ya ulinzi na Rio Ferdinand.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Daniel Gakuba