Algiers. Vyama washirika wa rais vyapata ushindi. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Algiers. Vyama washirika wa rais vyapata ushindi.

Vyama vitatu vinavyomuunga mkono rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria vimepata wingi mkubwa katika bunge kufuatia uchaguzi uliofanyika siku ya Alhamis.

Waziri wa mambo ya ndani Yazid Zerhouni amesema kuwa chama cha National Liberation Front FNL, Democratic National Rally na Society of Peace Movement kwa pamoja vimepata viti 249 kati ya viti 389 bungeni.

Hata hivyo, vyama hivyo vitatu vimepoteza viti 48, huku chama cha Nationalist FNL pekee kikipoteza zaidi ya viti 65.

Kiasi cha zaidi ya theluthi moja ya wapiga kura wamepiga kura zao katika uchaguzi wa Alhamis, umefanyika baada ya bomu la kujitoa muhanga mwezi uliopita katika mji mkuu Algiers ambapo watu 30 wameuwawa na wengine 200 wamejeruhiwa. Tawi la al-Qaeda katika Afrika kaskazini limedai kuhusika na mlipuko huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com