1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS : Rais Köhler yuko Algeria

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJj

Rais Horst Köhler wa Ujerumani anatazamiwa kufunguwa kikao cha Ushirikiano na Afrika leo hii kama sehemu ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini Algeria.

Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani Haidemarie Wieczorek –Zeul na wajumbe kutoka nchi nyengine wanachama wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo Makubwa ya Viwanda Duniani. Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo OECD na mataifa ya Kiafrika watashiriki kikao hicho.

Hapo jana Rais Köhler alikuwa na mazungumzo na Rais mwenzake wa Algeria Abdelaziz Bouteflika.Rais huyo wa Ujerumani pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano kati ya Ujerumani na Algeria juu ya usalama wa nishati na mabadilko ya hali ya hewa wakati wa ziara yake hiyo ya nne barani Afrika tokea ashike wadhifa huo wa urais hapo mwaka 2003.