Ajiripua kwa kubamiza gari dhidi ya basi la shule | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ajiripua kwa kubamiza gari dhidi ya basi la shule

ISLAMABAD

Mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amelibamiza gari lililosheheni mabomu dhidi ya basi la shule karibu na kambi ya kikosi cha anga kaskazini magharibi mwa Pakistan leo hii na kujiuwa yeye mwenyewe na kujeruhi watu tisa wakiwemo watoto watano.

Msemaji wa kijeshi Meja Generali Waheed Arshad amesema gaidi amelishambulia basi la shule ambapo dereva na mlinzi aliekuwa amekaa mbele wamejeruhiwa vibaya sana .

Shambulio hilo linakuja siku moja baada mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha kulibamiza gari lilosheheni mabomu kwenye kituo cha ukaguzi wa polisi katika bonde la Swat kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuuwa watu sita.

 • Tarehe 10.12.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CZiV
 • Tarehe 10.12.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CZiV

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com