Ahmadinejad azindua ndege iliyotengenezwa Iran
22 Agosti 2010Matangazo
Ndege hiyo yenye urefu wa mita nne imeonyeshwa hadharani siku moja baada ya kufunguliwa kituo cha nyuklia cha Bushehr kusini mwa nchi.
Kwa mujibu wa ripoti za televisheni ndege hiyo inayoruka bila ya rubani inaweza kubeba mabomu ya aina mbali mbali na kwenda masafa marefu na kwa kasi kubwa.
Ndege hiyo ni sehemu ya mipango ya Iran kutengeneza silaha zake zenyewe badala ya kutegemea nchi za nje. Israel na nchi za magharibi zinatuhumu kuwa Iran ina mpango wa siri kutengeneza silaha za nyuklia, lakini Iran inakanusha tuhuma hizo.
Mwandishi: P.Martin/ZPR
Mhariri: M.Dahman