1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afghanistan kuanza kampeni ya kutoa chanjo ya polio

24 Desemba 2023

Afghanistan itaanza kampeni ya kutoa chanjo ya polio kuanzia siku ya Jumatatu inayonuia kulinda zaidi ya watoto milioni 8.8 dhidi ya ugonjwa huo wa kupooza.

https://p.dw.com/p/4aXj9
Chanjo ya polio
Mtoto akipokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa polioPicha: Jose Aldenir/Zumapress/picture alliance

Wizara ya afya ya Afghanistan imesema kampeni hiyo itachukua siku nne lakini itaongezwa kwa wiki moja zaidi katika wilaya 42 mashariki mwa nchi hiyo ambapo kuna hatari kubwa ya kuenea kwa ugonjwa wa polio.

Watoto walio chini ya umri wa miaka 10 watapokea chanjo katika wilaya hizo 42 huku maeneo mengine ya nchi, chanjo itatolewa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano pekee.

Hivi karibuni, shirika la afya duniani WHO limetadharisha kuwa hatua ya kuwarudisha makwao wahamiaji kutoka nchi Jirani ya Pakistan imeongeza hatari ya kuenea kwa ugonjwa wa polio.

Waziri wa afya wa serikali ya Taliban Qalandar Ibaad amesema idadi ya wagonjwa wa polio iliyorekodiwa mwaka huu inatia wasiwasi. Ametoa wito kwa raia wote wa Afghanistan, wakiwemo wazazi kushiriki katika kampeni dhidi ya ugonjwa huo wa kupooza.