1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON 2013 : Cote D'Ivoire yaanza vizuri

27 Januari 2013

Katika mechi za kundi D zilizofanyika jana(22.01.2013),magoli ya dakika za mwisho kutoka kwa Gervinho wa Cote di'voire,na winga wa Tunisia Youssef Msakni yalizipatia ushindi timu hizo dhidi ya Togo na Algeria.

https://p.dw.com/p/17Q2Y
Ivory Coast's defender Emmanuel Eboue vies with Togo's forward Serge Gakpe during the 2013 African Cup of Nation in Rustenburg on January 22, 2013 at Royal Bafokeng Stadium in a Group D match. AFP PHOTO / ALEXANDER JOE (Photo credit should read ALEXANDER JOE/AFP/Getty Images)
Afrika Cup Tembo wa Cote D'Ivoir wakipambana na TogoPicha: AFP/Getty Images

Gervinho alihitimisha ushindi kwa timu yake inayopewa nafasi kubwa ya kushinda taji hili kwa goli lililofungwa katika dakika ya 88 na kuipatia Cote di'divoire ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Togo. Msakni alisubiri hadi dakika ya mwisho kuipa Tunisia ushindi wa goli moja dhidi ya mahasimu wao wa Afrika Kaskazini, Algeria.

Hadi sasa mechi tano kati ya nane zilizochezwa zimemalizika kwa sare, na tatu zimepata ushindi wa dakika za mwisho - Seidou Keita akiifungia Mali katika dakika ya 84 katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Niger siku ya Jumapili. Wakati ushindi wa jana Jumanne unamaanisha Cote di'divoire na Tunisia wako sawa katika uongozi wa kundi, walishinda katika namna tofauti.

Ivory Coast supporters hold up team scarves ahead of their team's African Nations Cup (AFCON 2013) Group D soccer match against Togo in Rustenburg, January 22, 2013. REUTERS/Mike Hutchings (SOUTH AFRICA - Tags: SPORT SOCCER)
Mashabiki wa Cote D'IvoirePicha: Reuters

Cote D'Ivoire yatamba

Cote di'voire ilishinda mchezo wa kufurahisha dhidi ya Togo wakati Tunisia na Algeria hazikuonekana kama zingefunga magoli hadi Msakni alipofunga goli maridhawa kutoka umbali wa mita 20.

Kitu zilichokuwa nazo timu mbili zilizoshinda ni kwamba hazikucheza vizuri kama zilivyotarajiwa. Cote di'voire ambayo nyota wake kama Didier Drogba, Kolo Toure, Didier Zokora na Emmanuel Eboue wanajaribu kwa mara ya mwisho kushinda kombe la mataifa ya Afrika walilolikosa tangu mwaka 1992, walifanya makosa kadha na walionekana kukosa mwelekeo.

Drogba mwenye umri wa miaka 34, alishindwa kuonyesha mchezo wa kuridhisha na alipumzishwa zikiwa zimesalia dakika 16 mchezo kumalizika. Mwenyewe alikiri kuwa mchezo ulikuwa mgumu, na kuongeza kuwa walifanya makosa mengi dhidi ya Togo. Shabiki  mmoja wa timu ya Cote di'Voire alisema.

epa03092182 Didier Drogba of Ivory Coast reacts after scoring the first goal of the match during the Africa Cup of Nations Quarterfinal match between Ivory Coast and Equatorial Guinea in Malabo, Equatorial Guinea, 04 February 2012. EPA/STR EDITORIAL USE ONLY +++(c) dpa - Bildfunk+++
Didier DrogbaPicha: picture-alliance/dpa

"Haikuwa rahisi, lakini Mwenyezi Mungu ametusaidia tukashinda mechi hii kwa magali mawili kwa moja".

Cote di'voire wamekuwa wakipewa nafasi ya kushinda kombe hilo katika mashindano manne yaliyopita, lakini wameshindwa kutimiza matarajio kila mara, wakipoteza katika mikwaju ya penati mwaka 2006 na 2012. hata hivyo, jana Jumanne walionyesha ubora unaohitajika na bingwa mtarajiwa - kwa kushinda mechi licha ya kucheza chini ya kiwango.

Nusura Togo ipate goli la  mapema

Togo ingeongoza mchezo baada ya dakika mbili pale nahodha wake Emmanuel Adebayor, alipopata nafasi akitumia makosa ya Kolo Toure. Lakini badala ya kufunga goli, alijaribu kumpiga chenga mlinda mlango Boubacar Barry, ambaye alifanikiwa kuuondoa mpira kutoka kwa mshambuliaji huyo. Shabiki wa Togo naye anaamini timu yake ilifanya vya kutosha.

Angola national football team supporters cheer before the Africa Cup of Nations (CAN) Group B football match between Ivory Coast and Angola in Malabo on January 30, 2012 at the Malabo stadium. Drogba will start the game from the bench, as a substitute. AFP PHOTO / ALEXANDER JOE (Photo credit should read ALEXANDER JOE/AFP/Getty Images)
Mashabiki wa AngolaPicha: A.Joe!AFP/Getty Images

"Nadhani Togo imejaribu kucheza vizuri, tumefanya tulichopaswa kufanya, na mimi bado ni Mtogo na najivunia kuwa Mtogo".

Selecção Futebol 03.JPG Titel: Fußball-Nationalmannschaft der Kapverden vor dem Spiel gegen Kamerun Ort: Praia, Cabo Verde Fotograf: Daniel Almeida Datum: 08.09.2012 Beschreibung: Das Team aus den Kapverden vor dem Qualifikations-Spiel zur Afrika-Meisterschaft gegen Kamerun. Die Kapverden gewannen das Spiel mit 2:0. Die Kapverden haben sich 2012 zum ersten Mal für eine Afrika-Fußball-Meisterschaft qualifiziert. Die Inselrepublik wird in Südafrika 2013 zum ersten Mal an einem Africa Cup of Nations teilnehmen.
Kikosi cha Cape VerdePicha: DW/Daniel Almeida

Mzunguko wa pili wa mechi hizo unaanza leo Jumatano(23.01.2023) ambapo wenyeji Afrika Kusini wanacheza dhidi ya Angola na Morocco ikipambana na visiwa vya Cape Verde katika kundi A katika uwanja wa Moses Madhida mjini Durban. Timu zote katika kundi hilo ziko sawa zikiwa  na  pointi moja baada ya sare mbili tasa mjini Johannesburg Jumamosi wiki iliyopita.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/rtre

Mhariri: Josephat Charo