ADDIS ABABA: Rais Mbeki ajiuzulu kama mpatanishi wa mzozo wa Ivory Coast | Habari za Ulimwengu | DW | 18.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA: Rais Mbeki ajiuzulu kama mpatanishi wa mzozo wa Ivory Coast

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amejiuzulu kama mpatinishi katika mzozo wa kisiasa wa Ivory Coast.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, rais Denis Sassou Nguesso, alisema rais Mbeki kwa hiari yake aliwasilisha pendekezo la kujiondoa kutoka kwa jukumu hilo.

Msemaji wa rais Mbeki, Mukoni Ratshitanga, amesema uamuzi huo umetokana na kuchaguliwa kwa Afrika Kusini kuwa mwanachama wa muda wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, hatua ambayo ambayo amesema itaitatiza kazi yake ya upatinishi.

Rais Dennis Sassou Ngweso amependekezwa achukue mahala pa rais Mbeki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com