ADDIS ABABA : Meles hahitaji kibali kushambulia Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 25.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA : Meles hahitaji kibali kushambulia Somalia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amesema leo hii nchi yake haitosubiri idhini ya kigeni kushambulia Muungano wa Mahkama za Kiislam katika nchi jirani ya Somalia jambo ambalo wengi wanahofia kuwa litapelekea kuzuka kwa vita vya eneo zima la Pembe ya Afrika.

Wakati muungano wa mahkama hizo za Kiislam ukimimina wanajeshi kwenye medani za mapambano nje ya makao makuu ya serikali ya mpito ya Somali inayoungwa mkono na Ethiopia kwenye mji wa Baidoa Meles ametaka uwelewa wa jumuiya ya kimataifa kwa jambo hilo lakini amesema haihitajii ruhusa ya kupigana.

Akizungumza katika mji mkuu wa Addis Ababa siku mbili baada ya kutangaza kwa bunge kwamba Ethiopia imekamilisha maandalizi ya vita amesema ameufahamu wa wito wa kutaka kujizuwiya na amejizatiti kwa mazungumzo lakini itachukuwa hatua kuihami nchi yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com