1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACEH: Mafuriko yasomba nyumba nchini Indonesia

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfG
Rais mpya wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akimuaga mtangulizi wake Jacques Chirac
Rais mpya wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akimuaga mtangulizi wake Jacques ChiracPicha: AP

Maafisa wa serikali ya Indonesia wamesema nyumba elfu kumi na tatu zilisombwa na maji wakati wa mafuriko ya hivi karibuni yaliyokumba jimbo la Aceh katika kisiwa cha Sumatra.

Watu takriban 200 wametoweka.

Serikali imetoa mashua na ndege za helikopta kupeleka msaada kwa watu 365,000 ambao wamepoteza makazi yao.

Nchi jirani, Malaysia nayo inajianda kwa mvua kubwa itakayoandamana na upepo mkali.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha uwezekano wa kuongezeka upepo mkali utakaosababisha mvua kubwa.