ACCRA : Steinmeir aamini mkutano wa Afrika na Ulaya kufanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 04.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ACCRA : Steinmeir aamini mkutano wa Afrika na Ulaya kufanyika

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amekamilisha ziara yake ya siku tatu barani Afrika kwa kuzitembelea Nigeria na Ghana.

Kabla ya kuondoka kwenye mji mkuu wa Ghana Accra Steinmeir ameelezea imani yake kwamba mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Afrika utafanyika kama ilivyopangwa.Waziri wa mambo ya nje wa Ghana Akwasi Osei Adjei pia amesema kwamba anatumai mkutano huo ambao utakuwa wa kwanza kufanyika baada ya miaka saba utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa licha ya uwezekano wa kuhudhuriwa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye yumo kwenye orodha ya watu wasiotakikana ya Umoja wa Ulaya.

Ureno mwezi uliopita ilishika wadhifa wa kupokezana wa urais wa Umoja wa Ulaya kwa kutangaza kwamba mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Afrika utafanyika mwezi wa Desemba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com