1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Mafuriko Bara Afrika yasababisha vifo 200

15 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPk

Zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha yao katika mafuriko yaliyotokea majuma ya hivi karibuni katika Afrika ya Magharibi na Kusini mwa Sahara.

Mafuriko hayo yameathiri zaidi ya watu milioni moja.Nchini Ghana kiasi ya watu 260,000 wamepoteza makazi yao,ambako mazao na nyumba zimeteketezwa kwa maelfu.

Ethiopia,Rwanda na Uganda pia zimeathirika vibaya.Umoja wa Mataifa unafikiria kupeleka tume ya kusimamia maafa.